ROSHAN HANDBAG'S

ROSHAN HANDBAG'S

Saturday, 28 February 2015

TANZIA: Captain John Komba afariki Dunia





Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni. 

Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kwamba Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Damian Komba amefariki dunia.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Kapteni Komba amefariki katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya sukari yaliyokuwa yakimsumbua.

Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) atakumbukwa sana kwa umahiri wa utunzi wa nyimbo mbalimbali za kwaya akiwa na TOT. 


Miaka mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini India alikokwenda kufanyiwa upasuaji kwenye nyonga, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu likichagizwa na ule unene aliokuwa nao.

Upasuaji huo ulilazimika kufanyika kwenye Hospitali ya Apollo kutokana na Hospitali ya Muhimbili kuathiriwa na mgomo wa madaktari wakati huo.


Alipofika India, madaktari walisita kumfanyia upasuaji kutokana na kuwa na mwili mkubwa hivyo wakamwambia kuwa asilimia za kuamka katika upasuaji huo ni ndogo lakini Komba akawasisitiza wamfanyie tu.


Tangu wakati huo, Komba alikuwa na kibarua kikubwa cha kupunguza uzito kwani awali alikuwa na kilo 138, lakini akajitahidi kupunguza hadi kufikia kilo 128 ambazo pia aliendelea kupunguza hadi kilo 100.

Mungu ailaze roho ya Marehemu John Komba mahali pema peponi, Amen.

                                     marehemu captain john komba





No comments:

Post a Comment